Tuesday, February 22, 2011

Majabali na vichaka huficha vitu adimu..

Kila Hifadhi ya hapa Tanzania ina utofauti na upekee wa aina yake. Utofauti huu unaleta utofauti wa namna na muda mzuri wa kuzitembelea na upatikanaji wa wanyama (kirahisi) ktk hifadhi hizi. Guides wazoefu wanakuwa na uelewa wa nini wakiangalie ili waweze kupata mnyama ambae mgeni wake ana hamu nae. Kwa wengi wetu, ile Big five huwa inawavutia wengi kuiona na wengi husuuzika roho zao baada tu ya kuona wale wanyama aliokuwa nao na kupata maelezo kadhaa anakuwa anamuona mnyama husika. Japo wapo wanyama wengine ambao nao ukikutana nao porini (ukiachia big 5) wanakuwa wanatoa msisimko wa kipekee kwa mgeni.

Kwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti vichaka na majabali (maarufu kama Kopjes - inatamkwa copies) huwa ni sehemu muhimu ya kupata Sharubu, wa chini na hata fisi. Isitoshe, kuna Kopjes ambazo zinafahamika kuwa na wanyama hawa. Hii inatokana na ukweli ya kwamba Sharubu ni wanyama wenye kumiliki eneo (territorial) hali ambayo huwafanya kuwa ndani ya eneo lao muda mwingi kwa usalama wao. Endapo eneo hilo likiwa maeneo yenye kopjes, basi hamta maliza kopjes nyingi kabla hamjawaona. Baadhi ya Kopjes zipo sehemu ambazo hamtaweza kuzisogelea karibu kama kibali chenu hakiruhusu kufanya off-road driving. Filming permit pekee ndio inatoa fursa na uhuru wa kufanya off road driving ktk National Parks. Kwenye Game reserves off road drving sio kosa - ruxa.
Pia sehemu nyingine kopjes zipo umbali mkubwa toka ilipo moja kwenda ilipo nyingne. hapo katikati unakumbana na uwanda wa nyasi ambao unaifanya Serengeti kuwa maarufu na upekee usio kifani Duniani.

Ukanda wa ziwa umezungukwa na miamba ya namna hii japo majina yake hutofautiana. Maeneo yaliyopo kando kando ya ziwa Victoria mawe haya hujulikana kama Bismark ilhali Serengeti yanajulikana kama Kopjes.

Hapa miti na miamba viko pamoja.

(Picha | Maktaba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment