Tuesday, February 22, 2011

Ngurdoto Crater - Arusha NP

Wageni toka nje wakifurahia na kushangaa Ngurdoto crater. Ngurdoto crater ni moja ya vivutio vilivyopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Arusha iliyopo mkoani Arusha (30kms toka Arusha mjini). Ngurdoto crater ina sehemu kadhaa (nje ya crater) ambako mgeni anaweza simama na kuangalia wanyama watakaokuwepo ndani kwenye crater kipindi hicho. Wengi tumeizoea Ngorongoro crater lakini Tanzania kuna crater nyingine kadhaa ambazo zinapatikana ktk ukanda wa kaskazini zenye hazina kubwa ya wanyama pori. Mojawapo ikiwa Empakaai iliyopo karibu na 'Mlima' wa Oldonyo Lengai. Jitihada mathubuti zinahitaji ili taswira kama hizi nyingi ziwe zimebeba nyuso za wazawa. Tofauti na hali ilivyo ambapo wageni toka nje ndio wanaonekana kutembelea na kuangalia vivutio vyetu. (Picha | Tanzania Giraffe Safaris)

No comments:

Post a Comment