Tuesday, February 22, 2011

Hutakiwi kuligusa, kulichukua au kulihamisha....

Kwa mujibu wa taratibu zinazosimamia uhifadhi ndani ya maeneo tengwa, ni kosa kwa mgeni kuchukua, kubeba au kuhamisha masalia ya manyama au wanyama hai waliopo ndani ya eneo la hifadhi. Mafuvu na mifupa vinaweza beba sura ya uchafu au kero mbele ya macho yako na yangu lakini kwa wahifadhi fuvu kama linaloonekana ktk picha juu lina nafasi yake ktk mfumo wa maisha ndani ya eneo husika. hapo kuna bacteria na wadudu kadhaa wanaoishi ktk hilo fuvu na kuendelea kubalance mfumo mzima wa chakula na mahitaji mengineyo ktk eneo. Jihadhari na vitendo hivi ili usiishie kubaya ukiwa ktk safari yako porini. (Picha| Ngorongor crater, TTB)

No comments:

Post a Comment