Thursday, February 17, 2011

Macho yake...

Wanyama wa porini wamepewa uwezo unaowawezesha kukabiliana na mazingira wanayoishi. Mathalan, wanyama wanaoishi kwenye maeneo ya baridi kali, wamepewa ngozi yenye manyoya na mafuta mengi ili kuweza kuwalinda na baridi hilo. Kwa wale wanaoishi maeneo yenye barafu wanakuwa na uwezo wa kuhifadhi chakula ndani yao ili kiwasitiri kipindi ambacho barafu imepamba moto. Wanyama wanaioshi ktk hifadhi zetu nao wamejaaliwa uwezo unaowawezesha kuishi na kustawi ktk mazingira yao. Duma (Cheetah) aka Wa Chini (kama anavyojulikana porini) amejaaliwa uwezo wa kukimbia kwa kasi sana. japo uwezo huu ni mzuri lakini una mahitaji yake ili uwe na manufaa kwa wa chini. Kuwa na mbio kunahitaji uwanda wa wazi ili wa chini aweze kuchanganya mbio zake na kushinda vitoweo anavyowinda. Ndio maana, wa juu hupatikana ktk hifadhi zenye uwanda wa wazi wa nyasi ambazo sio ndefu. Mazingira haya ni mazuri kwake kufanikisha mawindo yake.

Kama hufahamu, Wa chini hufanya mawindo yake mchana. hii humaanisha ni lazima awe na uwezo wa kuona mbali ktk mazingira ya jua kali. Wa chini anafanikiwa ktk hili kutokana na kujaaliwa kuwa na rangi nyeusi inayozunguka macho yake yote mawili. uwepo wa rangi hii nyeusi mbele ya macho yake humsaidia wa chini kuweza kuzuia makali ya miale mikali ya jua kutua machoni mwake moja kwa moja na kumzuia kuona akiwa ktk mawindo yake. Mbinu ambayo hutumika pia na wadunguaji au wanajeshi, japo wao hujipakaza rangi maalum nyeusi kuzunguka macho yao. Jua linapozama, wa chini huweka silaha chini na kutafuta sehemu salama kujificha ili asikumbane na wababe wa usiku (simba, chui, fisi na wengineo) ambao wanaweza kumdhuru. (picha | TTB)

1 comment: