Tuesday, February 22, 2011

Mkonga wake una kazi lukuki...

Mkongwa wa Tembo aka Masikio una kazi nyingi zikiwemo za kujihami na uvamizi wa namna yoyote. Masikio anautumia mkonga wake kupumulia, uchukuzi (kuchukua chakula na maji toka ardhini na kuyapeleka mdomoni) na mara nyingi kama mkono wa kufanyia shughuli zake mbalimbali za kila siku.
Ktk picha ya juu, Masikio huyu alikuwa anautumia mkonga wake kunusa harufu za mbali ili aweze kubaini kama ni harufu ya shari au mambo yapo shwari. Kwa mzoefu, hii ni ishara ya kukueleza ya kuwa masikio huyu amepata hisia ya uwepo wako na anaanza kudadisi ili kubaini nini afanye. Masikio wana uwezo mdogo sana wa kuona. wanategemea sana uwezo wao wa kunusa. Kutokana na uwezo wao kuona kuwa mdogo, huwa wanatabia ya kufanya kitu kinaitwa "mock-charging" (kutisha) kitu chochote ambacho wanakuwa hawakielewi. Hii ni hatua ya awali ya kujaribu kubaini hali ya usalama wake. Wakati mwingine, mashambulizi yanayofanywa na tembo dhidi ya mwanadamu yanakuwa na maelezo ya udadisi/kutishia zaidi ya kujihami. bahati mbaya ni kwamba udadisi wake huwa na maafa wakati mwingine. (Picha| TTB)

No comments:

Post a Comment