Friday, February 4, 2011

Enendeni na mkaijaze dunia...

Ni tafsiri ya Mdau Makoninde wa Tanzania Giraffe Safaris kwa jinsi alivyowakuta wanyama hawa ktk hifadhi ya taifa ya Ngorongoro mwaka jana. Ni dhahiri wanyama hawa wapo ktk utekelezaji wa agizo hilo kwa vitendo. Picha juu ni sharubu wakiwa ktk mchakato wa uzazi .Porini tendo hili hujulikana kama harusi. ukisikia guide wanazungumzia habari ya simba kuwa kwenye harusi basi jiandae kukutana na hali kama hii.

Bwana Afya nao wamo, kama wasivyopitwa na mzoga hata kwenye mambo haya nao inawalazimu kuwajibika. Wanyama kwa ujumla huwa na mambo mawili makuu ktk kipindi chao cha maisha. Kula na kuzaa (kuhakikisha kizazi kinaendelea kuwepo). Shughuli zao na mambo yao yote huelekezwa ktk kufanikisha mambo hayo mawili. Wanyama watahama toka eneo moja kwenda jingine ili mradi wawe na uhakika wa chakula kule waendako. Wanyama watafanya timing ya harusi zao ili watoto wao waje kuzaliwa kipindi chenye usalama kwao (watoto). Ukikuta wanyama wa porini wanapigana, basi moja ya sababu ya ugomvi huo itakuwa ni harusi au mlo. Migration ya Serengeti huwa inahusisha mambo yote mawili.

Siesta huwepo ili kurudisha nguvu. Sharubu huwa ktk harusi kwa kipindi cha zaidi ya siku tatu. ktk kipindi hiki chote, dume na jike huwa karibu mno na wala hawaendi mbali. Hukaa eneo moja, jambo ambalo linatoa fursa kwa wageni kuwaona kirahisi ktk eneo wanalokuwepo. Guide akiambiwa kuwa sharubu wapo kwenye harusi eneo fulani, basi ni lazima achape mwendo (kama wageni wake hawajaona sharubu) kuelekea huko kwani anakuwa na uhakika wa kuwaona ki urahisi. Sharubu wanapokuwa harusini, huacha shughuli zote na kujikita ktk harusi yao. Nadhani hata sisi binadamu tume-copy utamaduni huu wa sharubu wa kwenda honeymoon mbali na kuachana na shughuli zote nyinginezo tulizonazo. [Picha na mdau Makoninde wa Tanzania Giraffe Safaris

No comments:

Post a Comment