Tuesday, February 8, 2011

Mkurugenzi mpya wa idara ya Utalii

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii amemteua Bw. Ibarahim Mussa (pichani) kuwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kuanzia tarehe 01 February 2011. Uteuzi huo ameufanya kwa mujibu wa kifungu cha 6 (1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002.

Ibrahim A. Mussa (53) ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii tangu mwaka 1982 hadi sasa ambapo alifanya kazi katika ngazi mbalimbali, katika Idara ya Misitu na Idara ya Utalii. Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Utalii, Ibrahim A. Mussa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi anaesimamia Utafiti, Takwimu na Mafunzo katika Idara ya Utalii.

Bw. Mussa ana Shahada ya Uzamili (International Tourism Management) aliyoipata mwaka 2005 kutoka chuo cha Sheffield nchini Uingereza. Bw. Mussa anachukua nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutoka kwa Bi. Maria Mmari ambaye amepangiwa kazi nyingine.

No comments:

Post a Comment