Thursday, December 9, 2010

Zana za Kiboko....

Ukisikia mtu ameshambuliwa na Kiboko, basi ni vyema ukafahamu ya kuwa alikumbana na meno yanayofanana na hayo unayoyaona ktk mafuvu ya viboko hapo juu. Licha ya kiboko kuwa na meno makubwa na makali, kiboko sio mla nyama. Mashambulizi yake dhidi ya watu au wanyama wengine huwa ni ya kujihami.
Picha hii imepigwa ktk geti la Matambwe. Geti la Matambwe ni geti la kuingilia ktk pori la akiba la Selous lililopo ndani ya mkoa wa Morogoro eneo la Kisaki. Huko ndiko yalipo makao makuu ya wahifadhi wa pori la akiba la Selous. Hii inakuonyesha ni jinsi gani Selous ilivyo kubwa

No comments:

Post a Comment