Thursday, December 9, 2010

Ni kinga wakati wa mapigano...

Sharubu dume huwa na jukumu la kutoa ulinzi kwa kundi la majike analolimiki ktk himaya yake. jukumu ambalo humpelekea sharubu dume kupambana na madume wenzie mara kwa mara mapito yao yanapogongana au wale sharubu wasiokuwa na majike wakihitaji kumiliki majike. Inaelezwa ya kwamba, uwepo wa manyoya kwenye shingo yake, huwa ni kinga kwake dhidhi ya makucha ya sharubu wenzie wanapopambana. licha ya kwamba sio magumu lakini uwepo wake hupunguza makali ya kucha ktk mpambano.

No comments:

Post a Comment