Thursday, December 9, 2010

Unafahamu jinsi ya kuandaa hema lako?

Hema la camping linapokamilika huwa linaonekana simpo lakini maandalizi yake sio simpo ki-ivyo. Usipolijulia unaweza ukawa nalo na ukashindwa kuliandaa ipasavyo jambo ambalo linaweza kukupelekea kulala nje. Ili kukupa wigo mpana wa kujifunza na kufahamu, nakushauri uende google na kuandika "pitching a camping tent". Utapata articles lukuki zitakazokupa maelezo ya jinsi ya kuandaa hema lako. zipo nyingine zitakuelemisha hata jinsi ya kuchagua eneo muafaka la kuweka hema lako uwapo porini.
Picha juu ni mdau JSK (kulia) sambamba na wadau wengine wakiandaa mahema yao Simba public campsite iliyopo Ngorongoro crater. campsite hii ipo nje ya crater, kwenye kingo za crater - crater rim. Shukran ya picha mdau JSK

1 comment:

  1. Mimi nilikuwa naona ni kitu simpo kama kukunjua mwavuli kumbe kinahitaji uelewa wake. Ahsante kwa kuongeza maarifa yangu

    ReplyDelete