Tuesday, December 21, 2010

Melela Nzuri campsite

Baada ya muda wa kazi kuisha na kuweka majembe chini, Ijumaa iliyopita kundi la wadau kadhaa waliamua kwenda kula weekend yao porini na kuchagua kwenda kufanya camping ktk campsite ijulikanayo kama Melela Nzuri camp site. camp site hii ipo pembezoni mwa hifadhi ya taifa ya Mikumi. Takriban kilometa 70 tokea Msamvu, Morogoro. Kwa atakae penda kufanya camping awasiliane nao mapema ili kufanya booking. Vifaa vya msingi kwa ajili ya camping utahitaji kuwa navyo aidha wewe mwenyewe au muandaaji wa safari yako.

Kwa kuwa hakuna uzio kati ya hifadhi na campsite, iliwalazimu wadau kuwasha moto ili kuweza kuwafukuza wanyama wakali ambao wangeweza kuvamia sherehe yao bila mwaliko rasmi. picha juu ni baadhi ya wadau hao wakiwa busy kuuchochea moto ambao ndio uliokuwa kinga yao.
Ni nadra kuwakuta wazawa wakifanya camping. mara nyingi wageni toka nje ya nchi au raia wa kigeni wanaoishi nchini ndio huenda kupiga kambi hapo. TembeaTz inawapongeza wadau hawa kwa uamuzi wao wa kutembelea hifadhi ya Mikumi.

No comments:

Post a Comment