Friday, December 10, 2010

Lagoon Walk, Ras Kutani

Uwapo ktk Hoteli ya Ras Kutani, Lagoon walk ni moja ya mambo unayoweza fanya tena unafanya mwenyewe - peke yako. Pembezoni mwa hii hoteli, kuna lagoon ambayo inaingia mita kadhaa ndani ya nchi kavu na upande mwingine hukutana na Bahari has kipindi cha mvua ambapo maji huongezeka kwenye mkondo huo (lagoon). Chumbani kwako kuna kijitabu chenye maelekezo mengi kuhusu hoteli, huduma na taratibu zake. Moja ya shughuli zinazoelezewa ktk kijitabu hicho ni Lagoon walk. Licha ya kwamba unaifanya mwenyewe lakini kijitabu kinakuwa na ramani ya safari nzima na unapokuwa unafanya lagoon walk unakutana na vibao vyene maelekezo. Kwa ufupi, unapofanya lagoon walk unakuwa unaizunguka hotel kama ukiamua kufanya safari kamili. Japo unaweza geuza popote pale unapojiskia.

Picha hizi mbili za awali ni sehemu ya mwanzo kabisa baada tu ya kuacha mchanga wa pwani.

Upande wa pili ndipo ilipo hotel. Paa linaloonekana chini ya hizo palm trees ni moja ya vyumba vya Ras Kutani vinavyooneka ukiwa upande wa pili wa mkondo.

Lagoon inazidi kutokomea nchi kavu. hapa ni baada ya kuiacha pwani

unavyozidi kwenda mbele umbali toka pande mbili za lagoon zinapongua. pande zote mbili za lagoon Miti ya mikoko imeshamiri vyema.

No comments:

Post a Comment