


Sababu kubwa ya hoteli hii kumiliki uwanja wake wa ndege licha ya kwamba ipo karibu na dar ni kurahisisha usafiri kwa wageni wake baina ya Ras Kutani na hotel nyinginezo. Ras Kutani inamilikiwa na kampuni ijulikanayo kama Selous Safaris kampuni ambayo inamiliki hoteli nyingine 2; Jongomero (Ruaha NP) na Selous Safari Camp (SelousGR). Wengi wa wageni (hususan wanaotoka nje ya nchi) huandaliwa mpango wa kutembelea Ruaha na Selous ambako hukaa ktk hoteli zilizo chini ya kampuni ya Selous Safaris. Mara nyingi safari zao huanzia ktk hifadhi na mwisho wa safari kabla ya kurudi makwao, wageni huja Ras Kutani kupumzika ktk pwani hii na kuondoa uchovu wa safari za porini. Ili kuwapunguzia muda wa safari, kampuni ya Selous imeweka viwanja vya ndege ili wageni waweze kusafirishwa kirahisi toka hifadhi moja kwenda nyingine na mwishowe Ras Kutani kwa njia ya anga. hii haikuzii wewe mdau ambae unataka kwenda Ras Kutani kwa usafiri wako binafsi bila ya kutembelea maeneo mengine. Jambo la msingi ni kuhakikisha ya kwamba unafanya booking yako mapema kupitia wakala wako au kwa kutumia taarifa zilizopo ktk tovuti ya Selous Safari Company. Kwenye kila hoteli, tembelea sehemu ya gallery ujionee taswira maridhawa za kutoka ktk camp husika.
It seems to be a peaceful place.
ReplyDelete