Monday, November 8, 2010

Ilianza hivi.....

Iliingia garage ikiwa ni Land Cruiser mkonga - pick up. Ilipelekwa huko kwa lengo moja tu, kuibadilisha na kuifanya kuwa gari la safari

Bila hiyana, timu mahiri ya Hidden Treasure garage ya huko A-Taun waliifanyia ukarabati ndinga hii na kuitoa kama inavyoonekana ktk mtundiko ufuatao.

Ukiiona ndinga yako ikiwa ktk mchakato huu unaweza usiitambue au unaweza ukaumia roho kwa jinsi inavyosasambuliwa. Ndio maana baadhi ya garage zinakuwa zinazuia sana wenye magari haya kuyaona yakiwa ktk mchakato au hata kuruhusu mgeni kuingia eneo la kazi kuona nini kinaendelea. TembeaTz inaishukuru sana HTT kwa kuiruhusu itembelee garage yao na kujionea shughuli zinavyoendelea bila hiyana. Sehemu kadhaa tulizongonga hodi tulikosa fursa tuliyoipata HTT.

No comments:

Post a Comment