Monday, November 8, 2010

humtambua kwa harufu..

Baada tu ya kuzaa, bila ya kupoteza wakati mnyama huanza kumlamba kichanga wake. zoezi hili linaweza kupewa tafsiri ya usafi lakin ukweli ni kwamba wakati huu mama anakuwa anaanza kujizoesha harufu ya kichanga wake ili aweze kuja kumtambua siku zinavyozidi kwenda. Hili zoezi ni muhimu kwa wote, mama na mtoto. mama linamhakikishia kuwa atakuwa na uhakika wa kukilea kichanga wake mpaka umri wa kutengana utakapofikia (kulingana na aina ya mnyama) na kwa mtoto hiyo inamhakikishia supoti ya mama ktk malisho, ulinzi na mambo mengine ambayo mtoto humtegemea mamaye.

wanyama wanaokula nyasi hupendelea kuzaa kwa kipindi kimoja, hali ambyo hupelekea kundi kuwa na watoto wengi walio na umri unaofanana. Endapo mama atashindwa kumtambua mtoto wake, ni dhahiri wataweza kupoteana ktk mikingamo ya maisha ya kila siku. Mwanzo, utambuzi huu unakuwa ni one way traffic - mama ataweza kumtambua mtoto lakini mtoto atakuwa hawezi. baadae mtoto nae huwa na uwezo wa kuweza kumtambua mama yake. picha juu ni Ruaha NP, picha - TTB

No comments:

Post a Comment