Tuesday, October 26, 2010

Jike ndiye muwindaji...

Kwenye jamii ya Sharubu, sharubu jike ndie mwenye jukumu la kuwinda na kutafuta chakula kwa ajili ya kundi la simba wengine na watoto kama wapo. Dume huwa na jukumu kuu la kuhakikisha usalama wa kundi na watoto wake kutoka kwa madume wengine. sambamba na jukumu la 'harusi'.
Usije shangaa mara nyingi unapoangalia documentary zinazohusu wanyama wa porini ukakuta sharubu jike akiwa mstari wa mbele kusaka msosi. Mtundiko huu ni moja ya ushahidi wa hii dhana ambao mdau alimkuta sharubu huyu akiwa ameangusha nyumba na kuanza kumtafuna taratibu. japo hii haimaanishi ya kwamba dume hawindi, ukweli ni kwamba dume (hasa wale ambao hawana kundi nao pia huwinda ili kukidhi mahiaji ya matumbo yao.

Alikuwa yupo peke yake, hii ikiwa ni ishara ya kwamba sharubu huyu ni mwindaji mzoefu. alifanikiwa kumnasa nyumbu peke yake

Anapokuwa na uhakika ya kwamba hana mpinzani ktk mlo wake, sharubu huwa na mapumziko mafupi anapokuwa anakula. Ktk hifadhi ambazo kuna kuwa na miti na vichaka, sharubu anapofanikiwa kumwangusha mnyama, mara moja hupenda kuficha windo lake chini ya mti au kichaka ili asionwe na wengine. Fisi au sharubu toka kundi jingine pinzani huwa ndio adui zake. namba moja ktk matukio haya. Tabia ya kuficha windo chini ya mti huwanyima fursa tumbusi (tai) kuliona windo hilo na kuanza kumzonga toka hewani. hali ya kumzingira hewani huwa ni ishara kwa bwana afya ambae huwatumia tumbusi kama radar yake kwenye kuzengea mawindo ya wanyama wengine.

Picha zote zlipigwa ktk pori la akiba la Selous na mdau Tom wa Kima Safaris

No comments:

Post a Comment