Tuesday, October 26, 2010

Wengi huuzunika na hali kama hii....

Wazawa humpa nafasi ya kipekee twiga. hii hutokana na ukweli wa kwamba ndie mnyama kielelezo kwa taifa letu.

wazalendo wanapokuwa porini, hupatwa na simanzi wanapokutana na taswira kama hizi ambapo twiga anakuwa amegeuza kitoweo kwa namna moja au nyingine. Nilibaini hili ambao watu kama watatu hivi (mimi nikiwa mmoja wao) tulijikuta tukisononeka kuona mabaki ya twiga yakiwa yamezungukwa na tumbusi

Ukweli unabaki pale pale ya kwamba huo ndio mfumo wa maisha ya wanyama wa pori na kamwe sisi hatupaswi kuuingilia. endapo mnyama au wanyama wa jamii fulani watapungua au kutokomea ktk eneo, basi hautapita muda mrefu bila ya madhara ya upungufu huo kuanza kujitokeza. Aidha kwa kupitia mazingira au uharibifu wa namna yeyote ile. Japo ilitugusa, lakini ilibidi hayo yatokee ili mfumo wa ikolojia ya pori la akiba la selous uweze kuendelea kuwa ktk hali endelevu.

No comments:

Post a Comment