Wednesday, September 15, 2010

Tana 5, Special campsite; Serengeti NP

Mandhari ya Tana 5 campsite iliyopo ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti. Taswira hii inatoa mwanga wa mazingira ya campsite yanavyokuwa. Wageni huamua kukaa katika campsite aidha kwa kigezo cha kupunguza gharama au kwa kuwa karibu na wanyama na mazingira yao - adventure.

kuna campsite za aina mbili, Public na Special campsites. Special campsites ni kwamba kampuni yenye wageni hulazimika kufanya booking ya campsite mapema na kisha kufanya malipo. Baada ya hapo hakutakuwa na kampuni nyingine yoyoyte itakayoruhusiwa kwenda kutumia campsite ile (sepcial) mpaka pale yule aliye-book awali atakapamaliza muda wake. kwa public campsite ni kwamba kuna uwezekano mkawa wageni wa makundi tofauti tofauti lakin kila mmoja akiwa na mpango wake. Tana 5 ni special campsite.

Utakapoamua kukaa ktk campsite, inakulazimu uwe na vifaa vyako vya camping; mahema, vyoo na mabafu ambayo ni mobile sambamba na msosi wako mwenyewe. mbali na hilo itakulazimu uwe na mpishi (au wapishi - inategemea idadi ya wageni) wa kuhakikisha kuwa maakuli yanaandaliwa ktk hali na muda unaostaghili.

Kambi hizi huwa hazina umeme, ni mwendo wa kandili jua likizama ikibidi.

Ukitaka kufanya camping ni vyema uwasiliane na wataalam wenye uzoefu ili wakuandalie mpango mzima na wewe ubaki kufurahia safari.

Unapofanya camping katika campsite iliyopo ndani ya hifadhi ya taifa haupatiwi ranger (Askari wa wanyama pori) japo ranger huwa wanafanya patrol ktk hizi campsite kuangalia usalama wa wageni. ukifanya camping ktk pori la akiba, utapewa ranger wa kukusindikiza na kukulinda muda wote ambao utakaokuwa ktk pori husika.

Gharama za camping ni kama ifuatavyo:
Public campsite;
$30 - Raia wasio na uraia ktk nchi za Afrika mashariki
1,500 - Raia wa nchi za Afrika mashariki

Special campsite:
$50 - Raia wasio na uraia ktk nchi za Afrika mashariki
5,000 - Raia wa nchi za Afrika mashariki
Bei zote ni kwa mtu mmoja

Licha ya kwamba camping inaonekana kuwa na vikorokoro vingi, ni namna ya kukaa porini kwa gharama nafuu na kwa uhuru ukilinganisha na hotelini.
Shukran sana kwa mdau Tom wa Kima Safaris kwa picha hii ambayo aliipiga hivi majuzi alipokuwa Serengeti.
Kwa yule atakaependa kuandaliwa safari ya camping ktk hifadhi yoyote ile hapa Tanzania, anaweza fanya mawasiliano na mdau Tom kupitia thomas@kimasafaris.com

1 comment:

  1. Swala la camping itabidi lije baada ya kutembelea national parks mara kadhaa na kupata uzoefu wa mazingira ya huko. maana sasa hivi hata kulala nje kwenye misiba inakuwa issue, sembuse kulala porini!
    nawapa salute wale wanaomudu miki miki hii

    ReplyDelete