Friday, September 17, 2010

Kwanini migration ipo Serengeti peke yake?...

Nimeuliza wadau kadhaa swali hili na hapa chini ni moja ya majibu niliyoyapata toka kwa mmoja wa wadau niliowadodosa;

1. Ni kwa kuwa huku Serengeti wanakuchukulia kama breeding area especially southern part maeneo ya ndutu lakini kule masai mara inakuwa kama wanakutania kupata mimba tu
2. huku Serengeti kuna high concentration of phosphorus & calcium ambayo huchangia ukuaji wa watoto wa nyumbu
3. safety; Serengeti ni plain with short grass basi inakua ni mahali salama kwa nyumbu kuweza kujilinda na wanyama walao nyama (predators) na pia watoto wakizaliwa hawatapata buguza ya majani marefu katika ukuaji wao.

4. climatic condition; maeneo ya ndutu hadi olduvai gorge, kusini mwa Serengeti tuseme ni mazuri sana; ambapo hata kama ni kipindi cha mvua lakini panakuwa na joto flani ambalo litarahisisha uzalishwaji wa nyumbu
5. Nutritions; Serengeti ina high quality of grass na ni of high length pia sasa hivi sio kwa nyumbu tuu hata wanyama wengine walao majani wanavutiwa pia

6. Residents; wakati nyumbu wanahama kwende masai mara kuna wale wanaobaki kama residents. mara nyingi wanakuwa na rutuba nyingi especially madume na ndio wawapandapo majike hutengeneza mamba kwa haraka, ukumbuke
wanaobaki huku ni wengi kushinda masai mara, sasa hii hali huwafanya majike kurudi huku na kulowea huku sana
7. Food Chain; katika kubalance food chain ama tuseme eco-system ya chakula; nyumbu inabidi wawepo ili circle itimie. kama utakumbuka anayeanza juu ni twiga, wanafuata zebra na tembo then wao sasa kama wao wasipokuepo then wanyama wa chini kama swala na wengineo watakosa mlo bora.

N.B. Ikumbukwe kuwa wanakwenda masai mara kwa kipindi kifupi sana kulinganisha na uwepo wao huku Serengeti ni kwa kuwa masai mara iko under ikweta sasa inakuwa na mvua za kutosha na hivyo kufanya majani yawepo kwa kutwa nzima ya mwaka sasa Serengeti ni tropic so kipindi cha ukame kama utachunguza ndo utakuta wanahamia masai mara for greener pastures
Nadhani inatosha kwa leo

Mdau BB, Arusha

Dondoo zilizoifikia Tembeatz zinasema ya kwamba hivi sasa Migration ipo kaskazini mwa Serengeti, karibu na mto Mara njiani kuelekea nchi jirani kama inavyoelezwa ktk majibu ya mdau. Mchakato wa kuvuka mto mara huwa ni kitu kinachowavutia wageni wengi kuiangalia migration.
Blog yenu inajitahidi kunasa taswira kadhaa wakati wa kuvuka mto Mara. Shukran sana kwa Mdau BB kwa majibu na taswira. Lengo ni kupanua uelewa wa wengi ktk mambo yanayohusu hifadhi zetu na wanyama waishio ndani ktk hali inayomshirikisha kila mmoja.

3 comments:

 1. duu,nimekubali maelezo mazuri.Tunashukuru kwa kutufuambua macho

  ReplyDelete
 2. Nazidi kuongeza uelewa wangu kila mara ninapoitembelea blog hii.
  Ahsante sana kwa wadau wanaotumia nafasi hii kushare habari za national parks za hapa nyumbani

  ReplyDelete
 3. Kwa namna moja ama nyingine nimejifunza mengi kuhusu migration ahsante

  ReplyDelete