Saturday, September 11, 2010

Serengeti NP from Ngorongoro crater

Unapokaribia kufika geti la kushukia crater, ukiangalia upande wa kushoto unaweza kuona uwanda wa Nyasi wa Serengeti.

Jambo moja ambalo linaufanya ukanda wa kaskazini wa utalii kupendwa na wengi ni ukaribu uliopo baina ya vivutio muhimu. picha hizi sambamba na mitundiko mingine iliyotangulia, utabainisha ya kwamba unapokuwa ktk kivutio kimoja, kivutio kingine kinakuwa hakipo mbali. Mathalan, ukiwa Tarangire unaweza kuona Ziwa manyara. Ukiwa Ngorongoro, Serengeti inaonekana.
licha ya kwamba vivutio vilivyo ktk kanda nyingine za kitalii vipo mbali, ukweli unabaki kuwa na vyenyewe pia vina upekee wa aina yake na hazina kubwa ya mambo mazuri na ya kuvutia.

No comments:

Post a Comment