Sunday, September 19, 2010

Rock hyrax aka Pimbi

Wachache mwaweza mkumbuka yule kikaragosi aliyekuwa anatamba sana ktk majarida ya Sani aliyejulikana kama Pimbi. Alifahamika sana kwa mikasa aliyokuwa anakumbana nayo kila akiopoa. Zaidi ya hapo visanga vya wapenzi wake, Zena na Betina viliburudisha wengi. Ki ukweli wanyama hawa wanaofanana na sungura ndio pimbi wenyewe. Hupatikana sana ktk maeneo yenye miamba yenye mapango. ndio maana hata jina lao kwa kidhungu ni rock hyrax. Hawachezi mbali na majabali au miamba

Mdau Tom wa Kima Safaris aliwakuta hawa jamaa wakiota jua katika moja ya maeneo ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha hivi karibuni.

Picha zote zimepigwa hifadhi ya taifa ya Ruaha kwa ushirikiano wa Tom, Kima Safaris

1 comment: