Mdau alikutana na kundi hili la sharubu ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti aka Shambani. Picha hizi zimepigwa huko Serengeti hivi karibuni
Sharubu wa kushoto (aliyeinuka) alikuwa amevishwa kifaa shingoni. Ni dhahiri wanasayansi wanaofanya tafiti mbalimbali ndani ya hifadhi ya Serengeti, walimvisha ili waweze kufuatilia nyendo zake na kupata taarifa muhimu kwa ajili ya kuendeleza juhudi za kuwahifadhi wanyama hawa na maeneo wanayoishi. Ukifika ktk hifadhi na kumkuta mnyama kavishwa kitu shingoni usije dhania ni hirizi (picha: Mdau, Arusha)
No comments:
Post a Comment