Tuesday, September 7, 2010

Nyenzo ya kujikunia

Tembo aka Masikio, hutumia miti kama nyenzo ya kujikunia pale ambao muwasho wa wadudu unapozidi kiwango. wanyama wa porini wana namna mbalimbali za kupambana na wadudu wanaowabugudhi. Moja wapo ikiwa ni kujipaka matope ili kuwafanya mbung'o na wadudu wengine kushindwa kupenyeza mirija yao na kuwanyonya damu na kuwakera. Mbinu hizo zinaposhindikana kwa kukosekana tope au la, basi masikio hujisugua ktk miti kama hii ili kuweza kuwaondoa wadudu hao ktk miili yao.
Mti huu niliuona wakati wa safari za matembezi ya miguu (walking safari) ktk hifadhi ya taifa ya Tarangire mwezi juni mwaka huu.

No comments:

Post a Comment