Tuesday, September 7, 2010

kutoka Mto wa Mbu kuelekea Karatu; Manyara NP

Unapokuwa unatoka Mto wa Mbu kuelekea Karatu Ngorongoro mpaka Serengeti, Utapita mahali (baada ya geti la kuingia Hifadhi ya Manyara) ambako utakuwa kama unapanda mlima. Hapo utaanza kupata mandhari nzuri ya hifadhi ya Manyara (upande wa kushoto wa barabara) na msitu wake sambamba na ziwa Manyara lenyewe. Ki ukweli hapo upo ktk mchakato wa kutoka ktk sakafu ya bonde la ufa ndio maana unakuwa kama unapanda mlima. Msitu unaona ktk picha ya juu ni hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara huku ziwa Manyara likionekana kwa mbali.
Hifadhi ya Taifa ya Manyara ina upekee wake. Sehemu kubwa ya hifadhi hii ni msitu mnene wa miti ya migunga na miti mingine ya porini. Kwa Tanzania kila hifadhi ina upekee wake na kamwe mtu asikwambie ukiitembelea hifadhi moja, basi nyingine ni kama ile uliyoenda. huyo atakuwa anakubania uhondo! Fanya mpango utembelee hifadhi nyingi kadri uwezavyo ujionee hali halisi ilivyo na hazina ya maarifa unaoihifadhiwa ndani ya hizi hifadhi zetu.

Unavyozidi kuendelea na safari ndivyo unavyozidi kupanda juu na kujiweka ktk nafasi ya kuliona vyema ziwa Manyara. Mita kadhaa toka hapa kuna kituo maalum kwa ajili ya kuangalia na kujionea mandhari mwanana ya hifadhi ya Ziwa manyara , Ziwa Manyara na bonde la ufa (Escarpment view point). Ni sehemu ambayo ilinikumbusha sana jiografia ya shuleni kuhusu swala zima la the Great rift valley of East Africa.


Unapokuwa unaelekea Karatu, Kushoto kulia kwako ni mwinuko wa bonde la ufa kama unavyouona ktk taswira hii. Juu ya eneo hilo ndio kuna uwanja mdogo wa ndege wa Manyara. Runway yake inaishia mita chache tu kabla ya kuanza hili poromoko kwa huko juu.

Ziwa Manyara kwa mbali sambamba na kingo za bonde la ufa

No comments:

Post a Comment