Tuesday, September 7, 2010

Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu

Kiwanda hiki kipo pembezoni mwa barabara ya Arusha-Babati mpaka Dodoma. Ndio ile barabara ambayo itakufikisha Tarangire pia. Kipo kilometa chache baada ya kupita njia panda ya kuelekea Hifadhi ya Tarangire (Kibaoni). Ni moja ya viwanda vikongwe kwa uzalishaji wa mbolea ya phosphate hapa nchini.

Kikosi cha TembeaTz kilipita hapa wakati kikielekea Maramboi Luxury tented campsite pembezoni mwa ziwa Manyara kwa mapumziko baada ya mizunguko ya siku nzima ndani ya hifadhi ya taifa ya Tarangire. Habari za kiwanda hiki nilizisikia na kuzisoma ktk vitabu vya kiada ktk ngazi mbalimbali za elimu nilizopitia. Safari ya kwenda Tarangire ilinisogeza karibu na kukiona kiwanda chenyewe. Kuna mengi ya kujifunza uwapo ktk safari za utalii. Mengine ni nje kabisa ya utalii lakini ni hazina nzuri kwa uelewa wako juu ya taifa letu la Tanzania.

1 comment:

  1. KK, asante kwa Jiografia fupi ya kiliko kiwanda hiki. Nilivyo mie, nilikuwa nasikia kikitajwa Bungeni tu wakati wa vikao vya Mawaziri na Wabunge, lakini sikuwahi kufahamu hasa mahali kilipo, sasa wakizungumza, ninafahamu wanagusia eneo gani. THX.

    ReplyDelete