Tuesday, September 21, 2010

Mount Meru hotel kurudi ulingoni Novemba Mosi

Hizi ni picha zilizochorwa na msanii kuonyesha mandhari ya Hotel ya Mount Meru itakavyokuwa pindi ujenzi utakapokamilika na kufungua milango yake kwa wageni. Hoteli hii iliyopata kuvuma miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini inatarajia kufunguliwa rasmi mnamo mwezi Novemba mwaka huu. Itarudi tena ikiwa ktk hadhi ya nyota 5 na kuahidi ushindani mkubwa ktk sekta ya huduma za malazi ktk miji ya Arusha na Moshi.

Hoteli hii inatarajia kuajiri wafanyakazi takriban 300 ktk vitengo vyake mbalimbali.

Moja ya sehemu ya kupumzikia na mazungumzo itakavyokuwa ktk hotel hii

http://www.mountmeruhotel.com/

Unaweza kutembelea tovuti ya hotel hii na kujionea hatua zinazoendelea ktk ujenzi na pia kupata taaraifa zaidi. ktk sehemu ya news, kuna maelekezo kwa wadau ambao wangependa kujaribu bahati zao ktk kinyang'anyiro cha ajira ktk hotel hii. Shukran sana kwa Mdau Bonny toka Karibu Fair Arusha kwa kutuhabarisha mambo haya na mengine mengi.

1 comment: