Tuesday, September 21, 2010

Kiboko

Hupata mimba na hata kuzaa ndani ya maji. Dume moja hujimilikisha sehemu ya bwawa au mto na kuwamiliki pia majike wote wanaoishi ktk eneo hilo. dume huyu ndie mwenye ruhusa ya kuzaa na majike hayo. Madume wengine ni lazima wapigane nae, wampige na kumtimua ili nao waweze kuwa wakuu wa kaya. Licha ya kwamba madume wanamiliki maeneo ktk mito au mabwawa, nchi kavu kiboko hana chake. Ndio maana mara nyingi anapoona hatari, kiboko hugeukia ulipo mto na kuanza kutimua mbio kuelekea ulipo mto.
Porini, viboko wanajulikana kwa kuacha alama zinazoonyesha mapito yao. hufanya hivi kwa kuacha kinyesi ktk sehemu muhimu za mapito yao ili wasipotee wakati wa kurudi. Ukitembelea hifadhi ya Selous na kufanya walking safari pembezoni mwa mto Rufiji utajionea hali halisi ya hizi alama kando kando ya mto. Licha ya kuonekana ni kibonge, kiboko ana uwezo wa kutimua mbio kumzidi mwanadamu.
Ni Mnyama wa porini anaefahamika sana kwa kuwa na hasira na ndie anaeongoza kwa vifo vingi vya binadamu vinavyotokana na kushambuliwa na wanyama wa porini. Picha juu ilipigwa pembezoni mwa mto Ruaha, ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha. Shukran kwa mdau Tom, Kima safaris

No comments:

Post a Comment