Tuesday, August 24, 2010

Tulimkosa kiduchu tu...

Tukiwa njiani kurudi hotelini baada ya kuchapa mwendo ndani ya hifadhi ya Serengeti siku nzima (full day game drive), tulipofika karibu kabisa na hoteli tuliyofikia dereva alisimamisha gari ghafla na kutuuliza kama tumemuona wa-juu. Alipotuonyesha upande alipomuona wajuu huyo, haikuchukua muda wa-juu huyo akashuka toka juu ya mti aliokuwa ameupanda na kuingia kichakani. Kwa haraka haraka nilifanikiwa kuwahi camera na kunyakua taswira unayoiona hapo juu

Siku mbili baadae wakati tukiwa tunazunguka ktk maeneo ya hoteli tulimuuliza mmoja wa wafanyakazi kuhusu chui huyu ambae tulimuona chini ya kilomita mbili toka ilipo hoteli. Mfanyakazi yule alitujibu kuwa wa juu huyo yupo ktk teritory yake na huonekana mara nyingi sana na wageni maeneo hayo. Hususan mida ya jioni, mida ambayo na sisi tulimuona pia. Akasema kipindi cha kiangazi kinapogonga hodi, wa juu huyo hujongea maeneo pembeni ya bwawa la kuogelea la hoteli kwa lengo la kunywa maji toka ktk bwawa hilo mida ya usiku. Tulishukuru mungu kujua hilo siku ambayo kikosi kazi cha TembeaTz kilikuwa kina-check out ktk hotel na kuendelea na shughuli ktk mbuga nyingine.

No comments:

Post a Comment