Tuesday, August 24, 2010

Sabora tented camp - Grumeti reserve

Sabora Tented Camp ni moja ya hoteli tatu za kifahari zinazomilikiwa na kampuni ya Singita Game reserves. kwa hapa nyumbani, kampuni hii inasimamia pori la akiba la Grumeti, pori ambalo linapakana na hifadhi ya taifa ya Serengeti. Hoteli nyingine zinazomilikiwa na kampuni ya Singita kwa hapa nyumbani ni Faru Faru na Sasakwa zote zikiwa zimo ndani ya eneo tengwa la Grumeti

Tented camping ni namna murua ya kumsogeza mgeni karibu kabisa na natureKwa wale ambao wanashida ya uwoga, hapa vipi? unaweza kulala usiku kucha hapo? ha ha ha Hii ilikuwa ni kwa ajili ya kupiga picha za promo tu. Vingine vyote ni ukweli mtupu

Hoteli hii ipo ndani ya eneo la hifadhi lenye wanyama pori, hivyo mida mida wanyama huwa wanasogea karibu kabisa na hoteli na kukupa fursa mgeni kuwaona kwa karibu zaidi. Ieleweke ya kwamba shughuli zote ndani ya eneo la Grumeti zinasimamiwa na kuratibiwa na kampuni ya Singita game reserves. Tembelea tovuti yao kupitia www.singita.com kupata taarifa zaidi. Ahsante ya picha kwa Mdau Natalie wa Singita

2 comments:

  1. Kwa viwango vya bei ambavyo nimeviona kwenye website ya singita.com nadhani hii hoteli ni kwa matajiri zaidi.
    cha msingi ni kwamba nimeongeza uelewa wangu kuhusu grumeti reserve. asante kwa picha nzuri

    ReplyDelete
  2. Nice pics, truly luxurious

    ReplyDelete