Tuesday, August 24, 2010

Muonekano wa Oldeani toka Crater view point - Ngorongoro

Wengi tunapofika crater view point huwa tunakuwa na hamasa kubwa sana ya kuiona crater inavyoonekana toka hapo view point. Hamasa huwa kubwa kiasi cha kwamba huwa tunashindwa kuona mambo mengine mazuri ambayo yanapatikana hapo crater view point. Endapo utakuwa mdadisi na kugeuka nyuma na kuvuka barabara, utakutana na mandhari nzuri sana ya eneo lijulikanalo kama Oldeani. Eneo hili linakuwa linaonekana kwa chini huku wewe ukiwa juu kwenye milima ya Ngorongoro.

Ni Eneo ambalo ni maarufu sana kwa kilimo, mazao mengi (ya biashara na chakula) yanalimwa ktk eneo la Oldeani. Nakusihi mdau siku ukitembelea hifadhi ya Ngorongoro na kupata fursa ya kusimama crater view point, baada ya kukata kiu ya kuiona crater angalia upande wa pili wa barabara na kujionea mandhari mwanana ya eneo la Oldeani. Picha toka ktk maktaba ya TembeaTz

No comments:

Post a Comment