Tuesday, August 31, 2010

Oldupai Gorge

Ni Eneo ambalo wataalam wa mambo ya kale walifanikiwa kukuta mabaki ya mwanadamu wa kale na vitu vingine viliyoashiria uwepo wa mwanadamu ktk eneo hilo miaka mingi iliyopita. Kichuguu kinachooneka ktk picha juu hutumika kama kiwakilishi lakini eneo husika limesambaa ktk vituo kadhaa katika bonde hili. Ni Sehemu nzuri sana ya kwenda kujikumbusha baadhi ya vitu ambavyo wakati tukiwa shuleni wengi wetu tuliishia kuvikariri ili tufaulu mitihani. Picha hii niliipiga toka ktk moja ya vibanda ambavyo vimejengwa pembezoni mwa korongo la Oldupai mahali ambapo ipo makumbusho ya Oldupai.

Wengi tumezoea kuiita sehemu hii kama Olduvai (ikiwa na v) lakini ukweli ni kwamba jina au neno stahili la eneo hili ni Oldupai (ikiwa na p). mkanganyiko huu unatokana na wale wataalam waliofika eneo hili awali kuchanganya p na v kutokana na lugha za mataifa yao. Oldupai ni neno la kimasai lenye kumaanisha mmea wa katani mwitu. Mmea ambao umeshamiri sana ktk maeneo haya. Baada ya kugundua masalia haya, wataalam hao walihitaji jina la kulipa eneo (site name) husika kama taratibu zao zinavyoeleza. walipoomba msaada kwa wenyeji (Wamaasai), walipewa jina la Oldupai. Aliyekuwa anaandika notes wakati wa majadiliano hayo akaandika Olduvai badala ya Oldupai.

Eneo hili lipo ndani ye eneo la Ngorongoro conservation Area (NCAA) japo lenyewe lipo nje kabisa ya crater njiani kuelekea hifadhi ya taifa ya Serengeti. Ukiwa unatoka Ngorongoro kuelekea Serengeti kwa gari, Oldupai gorge ipo upande wa kulia wa barabara. Picha toka ktk maktaba ya TembeaTz; unaweza pata dondoo zaidi kwa kubofya hapa

1 comment:

  1. Jambo la Nyongeza:
    Hicho kichuguu unachokiona ktk picha hutumika kama ushahidi kuonyesha matabaka ya udongo yenye kuonyesha matukio mbalimbali ambayo yaliyotekea miaka ya nyuma ikiwemo Volcano za Ngorongoro ambazo zinaelezwa kuwa chachu ya Serengeti kuwa uwanda wa Nyasi kama ilivyo leo. Ni sehemu nzuri ya kujifunza (tena kwa kuona) mambo ya kale

    Kk

    ReplyDelete