Tuesday, August 31, 2010

Mikumi mwaka 2008

Kwa wale ambao hupata safari zinazopita njia ya Morogoro-Iringa, huwa na fursa ya kujionea mambo ya hifadhi zetu hususan Hifadhi ya taifa ya Mikumi. Wapo ambao wamediriki kusema wamewahi kufika Mikumi sababu tu alipita hapo akiwa njiani ktk barabara ipitayo katika hifadhi hii. Safari mahsusi ya kwenda porini ina mengi mengineyo ya kujifunza kuzidi ambayo mtu anayoyaona anapokatisha hifadhi ya Mikumi.
Mwezi Agosti mwaka 2008 nilipita hapo nikiwa safarini kuelekea mikoa ya nyanda za juu kusini.

Japo alikuwa mbali lakini ilitulazimu tupunguze mwendo ili kumpa heshima yake. Tukielewea vyema hapo ilikuwa ni ndani ya eneo la Hifadhi.

Huyu alikuwa karibu na barabara. Sijui nani alikuwa anamshangaa mwenzie hapa. Kipindi hiki hifadhi ya Mikumi ilikuwa ni kavu huku baadhi ya maeneo dalili za uwepo wa moto zikionekana waziwazi. Moto huu huwashwa na wahifadhi kwa kusudio la kuangamiza nyasi ndefu ambazo haziliwi na wanyama wengi na kutoa mwanya kwa nyasi mpya na fupi kuanza kuota. Ni moja ya shughuli ambazo wahifadhi hufanya ili kuhakikisha mzani wa mahitaji ya wanyama na mazingira unakuwa sawa.

Inakuwa ngumu kumuona mnyama kutokana na rangi ya mnyama kushabihiana na rangi ya mazingira. Hapa tulikuwa pundamilia kadhaa sambamba na swala paa wachache.

No comments:

Post a Comment