Tuesday, August 24, 2010

Kivuko cha mto Kilombero

Nchi yetu imejaliwa kuwa na mito mingi na mingine ikiwa ni mikubwa kushinda mingine. Mto Kilombero bila ubishi, ni mmoja wa mito mikubwa iliyopo hapa nchini. Hivi Karibuni Mdau AM alifanya ziara binafsi mitaa ya Kilombero na kuturushia taswira kadha wa kadha za zaira hiyo. Mtundiko huu ni baadhi ya taswira alizozipiga akiwa eneo la kivuko cha mto Kilombero. eneo hili hujulikana kama Kivukoni.

Licha ya kuwa ni eneo la kivuko, eneo hili pia ndio kama ni mpaka kati ya wilaya ya Ulanga na Kilombero. Aliposimama mdau wakati anapiga picha hii ni ndani ya wilaya ya Kilombero ilhali upande wa pili wa mto unauona ktk taswira juu ni upande wa wilaya ya Ulanga. Kwa kifupi, mto kilombero ni mpaka baina ya wilaya hizi. Eneo hili lipo ndani ya bonde la mto Kilombero, moja ya mabonde yenye rutuba na ardhi nzuri kwa matumizi ya kilimo.

pantoni inayotumika kuvusha watu na magari ktk mto huu ikiwa inafanya safari yake kuelekea upande wa wilaya ya Ulanga. Wilaya zote hizi zipo ndani ya mkoa wa Morogoro.

Mdau alipiga picha hii akiwa upande wa ulanga baada ya kuvuka. hapo ndio 'Ferry' yao, na magari unayoyaona yanasubiri pantoni ili iyavushe ili kuendelea na safari zake. Kilikuwa ni kipindi cha mbio za mwenge wa Uhuru na bango ulionalo lilikuwa na ujumbe wa kuuaga mwenge ktk wilaya ya Ulanga.
Shukran mdau kwa taswira na endapo kama kuna mdau mwenye taswira za maeneo mbalimbali zenye mandhari nzuri ya nchi yetu usisite kuzituma kupitia tembeatz@gmail.com

No comments:

Post a Comment