Hifadhi za hapa nyumbani ambazo zinakuwa na mito au mabwawa ndani yake huwa zinatoa fursa kwa wageni kuwa na nyongeza ya mambo wanayoweza kuyafanya. Ikiwemo kuangalia wanyama ukiwa ndani ya mtumbwi au boti. Huwezi kuizungumzia Selous GR bila ya kuutaja mto Rufiji, hiyo itakuwa sawa na kuzungumzia Misri bila ya kuutaja mto Nile. Mto huu umesambaa sehemu kubwa sana ya pori hili na kuliwezesha kuvutia wanyama wengi mwaka mzima kutokana na kuwa na uhakika wa maji na chakula.
Uwepo wa mto Rufiji ndani ya pori la akiba la Selous unakuja na gharama zake ikiwemo kubadili baadhi ya njia za mapito ya wageni kutokana na kujaa maji baada au wakati wa mvua. Kwa wengi ambao wamelitembelea pori la akiba la Selous baada ya kipindi cha mvua wanalijua hili. Jambo la msingi kuliangalia unapoamua kwenda Selous ni hali ya hewa. Kipindi cha mvua baadhi ya njia (vichochoro) hufungwa hivyo kufanya safari kufanyika katika barabara kubwa tu ambazo zimeshindiliwa vyema. Hii inakuwa inamnyima mgeni fursa ya kuona mengi kipindi. Licha ya hali hii, mgeni unaweza kuambulia jambo lolote kwani mambo haya huwa yana surprises zake. Ieleweke ya kwamba off-road driving inaruhusiwa ndani ya Selous kipindi cha Kiangazi.
No comments:
Post a Comment