Tuesday, August 17, 2010

Ukubwa wa gharama ndio kikwazo


Wadau,
hivi karibuni blog yenu ya habari na mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya utalii kwa hapa nyumbani ilijikita tena ktk mchakato wa kupata maoni yako ili kubaini chanzo kinachowazuia wazawa kuzitembelea hifadhi na maeneo tengwa yaliyomo ndani ya nchi yetu. Mchakato huu uliomalizika Jumapili jioni, ulifikia tamati kwa kigezo cha Gharama kuwa juu kupata mapendekezo mengi toka kwa wadau walioshiriki. Licha ya kutoa mwangaza huu, swala la kwanini wazalendo hawazitembelei hifadhi zetu kwa wingi kama wafanyavyo wageni toka nje ya nchi ni jambo ambalo linahitaji umakini na utulivu ili kulipatia ufumbuzi makini. Kwani licha ya wengi kuonyesha kuwa ukubwa wa gharama ndio chanzo, bado vipengele vya kutofahamu taratibu na mipango ya safari imeonyesho kuwa ni kikwazo pia. Kipengele cha kutojua utaratibu pia kilipata kura za kukiweka ktk nafasi ya pili baada ya kipengele cha ukubwa wa gharama.

Huu sio mwisho kwani ukweli ni kwamba kura hizi za maoni zimetoa ishiri tu ya moja ya sababu kubwa inayowafanya wazawa kushindwa kuzitembelea hifadhi zetu. Gharama ni eneo lenye mapana na marefu yake. Huu sio mwisho kwani tutarudi tena kwenu wadau ili kujaribu kufanya uchambuzi zaidi ili kupata suluhisho la hali ilivyo sasa.
Kama mdau utakuwa na maoni zaidi au hata tofauti, unaweze kushiriki kwa njia ya maoni (Comments ktk mtundiko huu) au hata kwa kutuma barua pepe kwenda email ya tembeatz@gmail.com

Shukran kwa wote waliotoa ushirikiano kwa namna mbalimbali ktk mchakato wa awali na huu uliokamilika hivi karibuni. Tunaomba ushirikiano huu udumu na kuendelea ktk michakato ijayo

Libeneke Juu....

No comments:

Post a Comment