Ni ktk Ngorongoro pekee ndio unaweza kukuta mchanyato huu ukiendelea bila ya madhara yoyote. Watu (Wa Kabila la Maasai) wakiishi na kuendelea na shughuli zao ktk maeneo ambayo yanakaliwa na wanyama pori pia, Ni aina ya uhifadhi ambayo kwa hapa Afrika ni Ngorongoro ndio mfumo huu unafanyiwa majaribio. Picha juu ni ng'ombe wakiwa ndani ya crater sambamba kabisa na pundamilia (mnyama wa porini).
Wamasai huishi nje ya crater (Lakini bado ndani ya eneo la hifadhi), Huwa wanaingia ndani ya crater kwa lengo la kupata maji kwa ajili ya mifugo yao. Safari zao za kuingia crater wakati mwingine hukutana na changamoto za wanyama wakali, lakini jamaa bado wanaendelea na utaratibu huu mpaka kesho

Mdau ukitembelea crater na kukuta ng'ombe, mbuzi au kondoo usije dhania nao ni wanyama pori. Mwenyewe hatakuwa mbali nao
Hili sikuwahi kulijua, shukran KK kwa kunifungua macho
ReplyDelete