Tuesday, August 31, 2010

Kundi la Makapera

Unapokutana na kundi la Swala na swala wote ktk kundi hilo wakiwa na pembe, basi jua kabisa kuwa hilo ni kundi la Swala madume ambao ni makapera. Katika jamii ya Swala, Swala dume mmoja ndie hutawala kundi kubwa la majike na watoto wao. yeye pekee ndiye mwenye haki ya kunaniihii nao ili kupata watoto. Swala dume anapozaliwa, hulelewa mpaka anapofukisha umri wa kubalehe nae hutimuliwa kundini. baada ya hapo swala yule mdogo huenda kujiunga ktk kundi la makapera walio jirani.

Lengo kuu la kila swala aliyeopo ktk kundi la makapera ni kwamba siku moja aje kumpindua swala dume anaetawala majike ili nae aje kupata fursa ya kuanzisha au kuendeleza uzao wake. Kwa kuwa mapinduzi ya swala huhusisha mapigano, daima swala kapera huwa anakuwa anajifua kwa mazoezi na mapigano yasiyo ya kweli (mock combat) baina yake na makapera wenzie. hii ndio inakuwa ni namna yao kujiweka ktk hali ya kuweza kuja kupambana na mtawala.
Kundi hili la makapera Lilikutwa na kikosi cha TembeaTz eneo njiani kuelekea hifadhi ya taifa ya Serengeti toka Ngorongoro.

No comments:

Post a Comment