Monday, August 2, 2010

Maasai Boma

Maisha ya jamii ya Wamaasai yana mengi ya kutufunza na kutuelimisha hasa kwa wale ambao tunaishi maisha ya kisasa. Ni kabila moja ambalo sehemu kubwa ya jamii yake imebaki kuendelea na kudumisha mila za mababu zao toka enzi na enzi licha ya wanajamii kutapakaa ktk kona mbalimbali za nchi yetu na dunia kwa ujumla. Kifupi, ichukulie maasai boma kama sehemu ya kwenda kuongeza uelewa na maarifa kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii.

Kuna wageni ambao hutoka nje ya nchi na kuja nchini kwa lengo la kuishi na jamii za Kimaasai kwa muda fulani. Ktk hili, mgeni hupokelewa airport na kupelekwa ktk Maasai boma (ambayo operator amemchagulia) na kumuacha huko kwa zile siku anazotaka kuishi huko. Lengo kuu ni kujifunza kwa kuona na kushiriki jinsi kabila hili linavyoendesha shughuli zake za kila siku.

Ndani ya nyumba ya mmasai (Ahsante ya picha - TTB)

No comments:

Post a Comment