Monday, August 2, 2010

Ni burudani na kujifunza

Unapoingia tu ktk maasai boma, utapokelewa kwa ngoma nderemo na vifijo kwa mila za kimaasai. Wanaume (morani) hujikusanya na kushusha show ya nguvu kukukaribisha ktk Boma mgeni wao.

Kina mama nao hawapo nyuma ktk kutoa burudani kwa mteja na kumpa maelekezo zaidi kuhusu maisha ya jamii ya Kimaasai ndani ya boma.

Ukitaka kupata fursa ya kunasa taswiraz zao wapo ambao watakupa fursa hii. Jambo moja la kujua mdau ni kwamba mambo haya yote yatakuhitaji kuzama mfukoni na kutoa chochote. Hii ni shughuli wanayoifanya ili mkono uweze kwenda kinywani. picha hizi zimepigwa ktk boma la Kimasaai iliyopo Ngorongoro crater karibu na getila kuingilia crater. Ahsante ya picha - TTB

No comments:

Post a Comment