Mchakato wa kura ya maoni umerudi tena, safari tukijaribu kubaini chanzo kinachowazuia wazalendo kwenda kutembelea hifadhi mbalimbali ambazo zipo hapa nchini. Hali ambayo imepelekea kujengeka kwa fikra za kwamba utalii ni kwa ajili ya raia wa nje tu.
Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuhusishwa na hali hii, kwa safari hii Tembea Tanzania imechagua vipengele vinne ambavyo tungependa kuviangalia. Vipengele hivyo ni;
- Kukosa Muda
- Gharamu kuwa kubwa
- Kutozifahamu hifadhi
- kutojua utaratibu
Tembea Tanzania imeamua kuchagua vipengele hivi (na kuacha vingine lukuki) kwa kuona ya kwamba vipengele hivi vinawakilisha maeneo makubwa muhimu yanayoihusu sekta hii na pia vipengele hivi vinapimika na kuweza kutolewa majibu yenye kujitosheleza.
Tembea Tanzania inakusihi kuendelea kushirikiana nasi kwa kushiriki ktk kura ya maoni hii ambayo ipo upande wa kulia wa blog. Chagua kipengele ambacho aidha ni kikwazo kwako au unadhani kinawafanya wazalendo wengi washindwe kuzitembelea hifadhi hizi za hapa nyumbani.
Kwa yule ambae engependa kutoa maoni zaidi, anaweza kufanya hivyo kwa kutoa maoni/comments kupitia mtundiko huu au hata kwa kutuandikia barua pepe kupitia tembeatz@gmail.com.
Pia kwa yoyote yule ambae ana taswira murua na angependa kushea nasi basi asisite kufanya hivyo kwa kutuma picha hizo kwenye tembeatz@gmail.com akitupa dondoo za taswira zake (wapi, lini na Nini kilimvutia).
Tunatanguliza shukran zetu za dhati na kukuomba tuzidi kuwa pamoja.
Karibuni sana, Libeneke juu.....

No comments:
Post a Comment