Monday, August 9, 2010

Kote kulikuwa ni mbali - Game walking, Maramboi

Baada ya kufanya game walking kwa muda kidogo, mimi na guide tulisimama na kujaribu kuangalia tumetembea kiasi gani. Ndipo nilipogundua tupo mahali ambako usalama upo mbali nasi.
Hotel ipo mbali na hata ziwa Manyara (kama lingeweza kutuokoa) nalo lilikuwa mbali nasi. Kwakuwa ari ya kulifikia ziwa Manyara ilikuwa juu, nilijikuta tukiendelea na safari yetu. Wakati mwingine walking safari huwa zinafikia tamati kwa vitu kama hivi, mgeni kukumbwa na woga wa ghafla na kuanza kuahirisha zoezi ili arudi mahala penye anapohisi pana usalama.

Ziwa Manyara likionekana kwa mbali tokea mahali tuliposimama kwa muda kufanya tafakari. Ki ukweli Game walking safari huwa ni activity nzuri kujifunza mambo mbalimbali ya porini. Taswira zote ni toka ktk maktaba ya TembeaTz.

No comments:

Post a Comment