Hivi karibuni Nilipokuwa pembezoni mwa Ziwa Momella dogo nilishuhudia wadau wakiwa ktk hatua za mwisho za kumaliza cannoe Safari aka safari za mitumbwi ndani ya Ziwa hilo. Safari hizi hufanywa chini ya usimamizi wa guide mzoefu kwa sababu za kiusalama. Picha juu ni mitumbwi miwili ambayo ilikuwa ikija pembezoni mwa ziwa kukamilisha safari yao.
Cannoe safari hutoa fursa kwa mgeni kujionea wanyama na mazingira yanayolizunguka ziwa Momella dogo huku akiwa ktk mtumbwi. safari hizi hazina tofauti sana na boat safari zinazofanyika Selous. Tofauti moja iliyopo ni kwamba kule Selous boat zinazotumika huwa na injini ilhali hizi za Momella ni mwendo wa makasia.
Mgeni akiwa sambamba na guide wake wakielekea eneo pembezoni na ziwa ambako walikuwa wameacha magari na vifaa vyao vingine.
Maelezo niliyoyapata ni kwamba safari hizi zinakuwezesha kuwaona Twiga, Tembo, aina mbali mbali za swala, ndege (wa Majini na hata wa nchi kavu) wapaokuja kunywa maji ktk ziwa hili. Japo inasisimua lakini inaelezwa ya kwamba kuna uwezekano wa kukutana na Chatu wakati wa safari hizi za mitumbwi. Ziwa hili lina viboko japo ni wachache. Kwa kuwa viboko ni wanyama wenye kujenga himaya (Territorial), waongozaji wanakuwa wanaelewa maeneo ambayo sio himaya ya viboko na ndio hayo huwa yanatumika kufanyia safari hizi. Siku hii tulisikia ngurumo za viboko japo hatukubahatika kuwaona na kunasa taswira zao.
No comments:
Post a Comment