Tuesday, August 24, 2010

Kuelekea Arusha NP

Picha juu ni njia panda maneo ya Usa River ktk njia ya Arusha Moshi. Kushoto ni njia kuelekea Arusha NP pamoja na Ngurdoto Mountain lodge. Ukinyoosha moja kwa moja unakuwa unaelekea Moshi. Toka hapa mpaka geti la Ngongongare ni kilomita 6.

Ukishaachana na njia ya Moshi-Arusha unakuwa umeingia ktk hii barabara ambayo inakupeleka moja kwa moja mpaka lilipo geti la Ngongongare ktk hifadhi ya taifa ya Arusha National park.

Utakutana na mandhari mwanana ya miti mirefu pamoja na mashamba ya kahawa kila upande wa barabara hii.

Utafika mahali Takriban kilomita 1.5 kabla ya kufika ktk geti lenyewe, utaachana na lami. kuanzia hapo barabara ni ya vumbi lakini iliyoshindiliwa vyema. Picha juu ni 'goli' linaloashiria kuwa unaanza kuingia ndani ya eneo la hifadhi. Majengo unayoyaona kuli kwa barabara ni maduka ya vitu mbalimbali vya asili zikiwe picha na vinyago mbalimbali mahususi kwa wewe, mimi na yule anaetembelea hifadhi hii.

Picha za tingatinga unazoziona kuli zinauzwa ktk duka lililopo hapo. Hapo ni nje ya eneo la hifadhi licha ya kwamba ndegere, nyani, twiga na swala hufika mitaa hii. Geti la ngongongare lipo mita chache baada ya kulipita goli hili.

No comments:

Post a Comment