Tuesday, August 24, 2010

Kibaoni - Njiani kuelekea Tarangire

Ukiwa unaelekea hifadhi ya Tarangire toka Arusha, utafika eneo lijulikanalo kama Kibaoni. eneo la Kibaoni lipo baada ya kupita eneo la Makuyuni ukiwa unaelekea babati-Dodoma. Ukifika kibaoni, hapo utalazimika kuelekea kushoto na hapo ndio utakuwa mwisho wa kukutana na lami. Njia ya Vumbi iendayo kushoto ndio itakayokupeleka ktk geti la kuingilia hifadhi ya taifa ya Tarangire. Ukiendelea na njia inayonyooka huko utakuwa unaende babati na kuendelea mpaka Dodoma. Si mbali na Kibaoni utakutana na kiwanda cha mbolea cha Minjingu.

Kibao chenyewe ambacho kinafanya eneo hili kujulikana kama Kibaoni.

Licha ya kwamba barabara sio ya lami lakini imeshindiliwa vyema hali ambayo inayoifanya iweze kutumika ktk vipindi vyote vya mwaka.

1 comment:

  1. KK,
    nakupongeza kwa kazi nzuri ya kutuelimisha na kutupa habari mbalimbali zinazohusu hifadhi zetu.
    Mimi ni mmoja wa wale ambao huwa nikiingia ktk mtandao, blog yako ni moja ya blogs ambazo huwa nazitembelea ili kujua mambo zaidi.
    Japo sijabahatika kutembelea hifadhi yoyote hapo nyumbani, lakini kwa kutembelea na kufuatilia posts ktk blog yako nimekuwa najiona kama nimefika vile.Endeleza kazi nzuri, wadau wako tupo sambamba nawe

    Huu mtundiko wa tarangire umenifanya nihisi kama vile nimeshafika kwa jinsi ulivyoelezea safari toka Arusha mpaka hapo kibaoni na kuendelea.
    Ipo siku nami nitaijipanga nisogee ktk moja ya hizi hifadhi za hapa nyumbani.

    ReplyDelete