Tuesday, August 10, 2010

Faru Faru Lodge - Grumeti Game Reserve

Faru Faru Lodge ni moja ya lodges ambazo zinamilikiwa na kampuni ya Singita Game reserves ambayo ndio inayosimamia na kuendesha pori tengwa la Grumeti aka Grumeti game reserve. Faru faru ni moja ya hoteli tatu zilizojengwa ndani ya pori tengwa la Grumeti. pori hili linapakana na hifadhi ya Taifa ya Serengeti eneo ambalo migration ya Serengeti huwa inapita pia. Picha juu ni moja ya vyumba vya hadhi ya juu vilivyopo Faru Faru Lodge.

Sio lazima upande gari na kwenda mwendo mrefu kuwatafuta wanyama. Tokea ukiwa kitandani unajiandaa kuamka unakuwa unapata view nzuri ya bwawa la maji ambalo mara nyingi huwa linakuwa na wanyama wanaokuja kunywa maji. Chumba kinakupa mandhari murua ya eneo ukiwa kitandani kwako.

Ukiwa bafuni nako mambo ni powa pia. Unakuwa unaoga huku ukipata mandhari maridhawa ya pori tengwa la Grumeti.

Hii ni sehemu ya wageni kuweza kupata taarifa mbalimbali na pia kujisomea vitabu kadhaa ambavyo vipo hapa. Eneo hili mgeni anaweza pata news mbalimbali kwa TV na hata mtandao wa Internet. Kwa ujumla eneo lote la hotel lina Wi-Fi internet ambayo mgeni anaipata buureee....

Bwawa la kuogelea ambalo nalo linakupa nafasi ya kuwaona wanyama na kufurahia mandhari ukiwa ktk bwawa hilo.

Mgahawa

Endapo ukipenda kula chakula chako porini (ndani ya pori tengwa la Grumeti) basi msosi wako utaandaliwa kwa style kama hii.

Jua likizama kuupisha usiku kuchukua nafasi yake. Wapenzi wa taswira za Machweo najua taswira hii itakuwa imewagusa kimtindo. Mimi ni mmoja wao

Night Game drive. Hii ni moja ya huduma ambayo unaweza kuipata ndani ya pori tengwa la Grumeti. Mgeni unakuwa unatembezwa porini kuangalia wanyama muda wa usiku. Kwa hapa nyumbani mizunguko ndani ya hifadhi (kwa wale wasio wahifadhi) inalazimika kusitishwa ifikapo saa 12 jioni. Hii inamaanisha muda huu ukifika aidha uwe umeshatoka nje ya hifadhi au umeshafika hotelini kwako. Wasimamizi wa pori tengwa la Grumeti wameruhusiwa kufanya shughuli hii (night Game drives) ndani ya eneo la Grumeti. Shughuli hii inatoa fursa kwa mgeni kujionea na kujifunza tabia za wanyama pindi jua linapozama. Unakuwa na nafasi ya kuona baadhi ya wanyama ambao mchana huwa wanajificha na hata kuwaona wale wanyama ambao mchana wanaonekana wajanja lakini jua likizama wanakuwa hawana ujanja tena.
Shughuli zote za utalii ndani ya pori tengwa la Grumeti huwa zinasimamiwa na kampuni ya Singita Game reserves yenyewe.
Bofya hapa ukipenda kujua zaidi kuhusu Faru Faru lodge na pori tengwa la Grumeti
Ahsante ya picha, mdau Bonny wa Karibu fair Arusha

2 comments:

  1. KK, wewe wajua ugonjwa wangu, tayari nimeichukua picha hiyo. We ukipoteza picha zako zote za machweo na mawio ya jua, utazikuta nakala zake kwangu.
    Shukrani sana kwa taswira mariddhawa!

    ReplyDelete
  2. Wallahi nasikia raha mie, nikiona mazingira haya hata kwenye picha tu.... ngoja nifanye mpango sijaona mazingira haya siku nyingi kidogo.

    ReplyDelete