Ni muendelezo wa taswira za mchakato ambao Land cruiser na magari mengineyo hupitia zinapokuwa zinafanyiwa modification kwa ajili ya matumizi ya safari za porini. Kama nilivyo dokeza awali, Sehemu kubwa ya nyuma ya gari hizi huwa zinaondolewa na kisha body mpya husukwa. Hususan kwa yale magari ambayo mwenyewe anataka liwe na uwezo wa kubeba abiria 7-8 au liwe na nafasi zaidi kwa wageni kukaa kwa raha na mustarehe. Picha juu ni jinsi hali inavyokuwa baada ya body liyokuja na gari garage kuondolewa na kazi ya kuvisha body mpya ndio inakuwa inaendelea.
Hapa ikiwa katika hatua za awali za 'kuivalisha body mpya' gari hii ili ije kuwa na uwezo wa kuhimili mikiki ya safari za porini.
Body mpya ya nyuma inavyoonekana kwa karibu baada ya kusukwa na kufungwa ktk ndinga. Hii ni Land cruiser mkonga ambayo ilikuwa inafanyiwa manjonjo ili ije kuwa warbus.
Mara nyingi mabadiliko haya hufanywa ili kuweza kumfanya mgeni akae kwenye gari kwa raha na mustarehe. Wapo wageni ambao hukaa na gari kwa tarkiban siku 20 mpaka 30 wakiwa ktk mizunguko mbalimbali ya porini. ktk mazingira haya, gari anayoitumia mgeni huyu lazima iwe na nafasi itakayomuwezesha mgeni kukaaa kwa raha na kufurahia safari. Ndio maana hizi gari huwa zinafanyiwa manjonjo ili kuzipa uwezo huu. Kwa yule ambae atafanya safari ya siku 1 au 2 hata ona tofauti lakini safari ikizidi siku nne na gari likiwa halina nafasi ya kunyoosha miguu, kusimama na kupata view nzuri huwa inakuwa inachosha.
Picha zote kwa hisani ya Workshop ya HTT-Safaris ya Arusha.

No comments:
Post a Comment