Friday, April 9, 2010

Sharubu wa Naabi Hill

Hawa ni Sharubu ambao hupatikana nje kidogo ya gate la Naabi Hill. Ukiwa unaingia Serengeti, unaanza eneo ambalo ni himaya ya hii pride kabla ya kulifikia gate la Naabi hill. Siku hii tuliwakuta wameangusha mnyama, wameshamla na kilichokuwa kinafuata ni usingizi mnono. Juu ni moja ya madume ktk kundi hili la Simba.

Alikuwa na partner wake.

Ukiuona huo mti unaweza sema usogee kwenda kujikinga na jua kali. Ukiangalia vizuri utaona tayari kuna sharubu jike 2 wameshawahi kushika nafasi hapo.

Madume walikuwa wengi kidogo ktk hili kundi siku hii. Yawezekana msosi ulikuwa ni starter so majike yalikuwa yameshaingia mzigoni kwenda kutafuta main course. Kwa Simba jike ndiye muwindaji na Dume yeye ni mlinzi wa himaya. Unaweza jikumbusha kuhusu mtundiko wa awali kuhusu Naabi Hill kwa kubofya hapa.

No comments:

Post a Comment