Thursday, April 8, 2010

Mandhari ya Horombo Hut - Kilimanjaro

Kibao kinachokukaribisha Horombo huts ukiwasili. Horombo ipo Mita 3720 juu ya usawa wa bahari.


HIvi ndio vyumba wanamolala wageni, Kibanda kimoja mnalala watu wanne.

Endapo mgeni atazidiwa na fweza yake inaruhusu, basi Horombo Hut kuna sehemu ya kuwezesha hedi-kopta kutua na kumpeleka sehemu ambayo atapata huduma zaidi. Kwa kawaida, mgeni akizidiwa kiasi cha kushindwa kutembea mwenyewe, kuna machela zao spesho ambazo porters watatumia kumshusha mgeni wao mpaka chini ili ahudumiwe. Jikumbushie mtundiko kuhusu toli toli za mlima kilimanjaro kwa kubofya hapa

wakati mgeni unalala ndani ya vibanda (huts) team yako - porter na guide - wao wanakuwa wanalala nje kwenye tents unazoziona.

Mdau akipelekwa chumbani kwake baada ya ku-check in Horombo hut.

Mandhari ya Horombo hut jua linapoelekea kuzama. [Picha: Mdau]

1 comment:

  1. Mdau,
    Unafanya a good good good job. Hivi vitu wengine tulikuwa tunaviona kama ni vitu kwa ajili ya wageni.

    Utafika wakati watanzania watapata mwamko wa kuupanda mlima Kilimanjaro sambamba na wageni. Huku nilipo (Sweden) nimewahi kukutana na jamaa 2 ambao waliupanda huu mlima mwaka juzi. Walifurahia sana na wamesema wanajipanga kurudi tena. Walishangaa sana kuona mimi sina hata mwamko wa kuupanda Mlima Kili ambo upo nchini kwetu. Sasa hivi hamu inaanza kunijia kwa mbali, Siku nikirudi home kwa likizo, nitaangalia uwezekano wa kuupanda

    Keep up the good work that you are doing.

    Mdau Sweden

    ReplyDelete