Thursday, April 8, 2010

Mandara Hut kwenda Horombo Hut - Kilimanjaro

Safari yetu kuelekea kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro inaendelea, safari hii tunapata dondoo za fungu la safari hii tokea Mandara Hut kueleke Horombo Hut. Sehemu kubwa ya fungu hili inakuwa ni ktk sehemu ya wazi tofauti na fungu la kutoka Marangu kuja Mandara ambako ni Msitu kinamna. Hata Uoto (Vegetation) ya hapa inakuwa tofauti na kule kwa mwanzo.

Uoto wa huku ni uoto wa milimani, Nyasi na miti unayoikuta huku, inapatikana zaidi maeneo ya milimani ambako kuna unyevu unyevu muda mwingi wa mwaka.

Ukiona mti unakuwa na kambakamba kama unaouona ktk picha juu ni dalili ya kwamba hapo ulipo ni eneo la baridi kali na tena upo juu tokea usawa wa bahari. Kwa Mbali ni Kilele cha Mawenzi kikiwa kimefunikwa kwa mawingu.

Hizi ndizo njia zenyewe wanazopita wakati wa kupanda na kushuka. Hii ni kwa wale wanaopanda kwa Marangu route.


Moja ya madaraja yaliyopo njiani ukiwa unaelekea Horombo, hili ni Daraja la mwisho kabisa kabla ya kufika Horombo hut.
[Picha: Mdau]

No comments:

Post a Comment