Saturday, March 20, 2010

Masikio

Kwa ile lugha ya Porini, hawa jamaa huitwa MASIKIO. Ni dhahiri picha juu inaelezea hilo jina walilopewa na wazee wa pori. Tembo wanagawanywa ktk makundi mawili, tembo wa africa na wale wa Asia. wa Africa inaelezwa ndio wenye umbo kubwa ukulinganisha na wale walio bara Asia. Kinachoweza kuwatofautisha kirahisi ni ukubwa wa masikio yao. Hawa wa huku kwetu wana masikio makubwa, ilhali wale wa bara Asia ya kwao ni madogo kimtindo.

Anapokuwa ametanua masikio yake kama hao juu, ni dhahiri kuna kitu kinamshangaza na anaanza kujihami kwa kupanua masikio yake ili 'adui' amuone yeye mkubwa kiumbo. ukiachia hili la kuonyesha dominance, tembo hupepea masikio yake ili kuweza kurekebisha joto la mwili. damu ya moto hupitishwa kwenye masikio ambako kuna ngozi laini na yenye mishipa midogo midogo ya damu. Mishipa hii huleta damu 'ya moto' kwa nia ya kupunguza joto la mwili na kisha kuirudisha mwilini kuendelea na mzunguko mwingine ikiwa imepunguzwa joto lake. kw anjia hii Tembo anakuwa anaratibu joto la mwili wake.
Hii tabia ya kupoza mwili kwa kutumia masikio ndio inayoelezwa kuwa chanzo cha tembo wa huku kwetu kuwa na masikio makubwa na wale wa bara Asia kuwa na madogo. Hii inatokana na ukweli kwamb sehemu kubwa ya maeneo ambako temba wanapatikana ktk bara la africa kuna hali ya joto, hivyo wanahitaji masikio makubwa ili kuweza kupooza miili yao. Wa Asia hawahitaji sana hii cooling mechanism kwa kuwa wapo ktk maeneo yenye hali ya ubaridi tofauti na huku.

Mkonga wake hutumika kuchumia nyasi na kisha kuzipeleka mdomoni, kushikia miti na kadhalika. kazi nyingine ya mkonga ni kuutumia ktk zoezi la kunywa maji. Tembo huvuta lita kadhaa za maji na kuzihifadhi kwa muda ktk mkonga wake. baada ya hapo huupeleka mdomoni mkonga wake na kisha kuyamiminia maji hayo mdomoni mwake. Tembo hatumii mkonga wake kama mrija. Ieleweke ya kwamba Tembo hupumua kwa kupitia mkonga wake pia. Hali ambayo humfanya kuutumia mkonga wake kupumulis, kunusa na kutambua harufu. tembo ktk picha juu kulia anaonyehs hali ya kunusa harufu ya kitu kilicho mbali nae ili kuweza kujua kama ni msosi au adui.

Masikio hupenda kuishi ktk makundi, na ktk makudi yao Jike mmoja ndio huwa kiongozi wa kundi hilo. kwa kawaida huwa ni Jike lenye umri mkubwa kushinda wengine ndio hupewa jukumu la kuongoza kundi la tembo.

Inaelezwa kwamba hivi sasa adui mkubwa wa tembo ni sisi ambao tunawawinda kiharamu kwa ajili ya pembe zao ambazo zina matumizi mbalimbali. Porini, tembo mkubwa na ambae afya yake haina mgogoro, hana mbabe. Simba sometimes huvizia na kudondosha tembo watoto japo hizi attempts huwa ni risky sana. Tembo hulinda watoto wao kwa gharama yoyote ile. Hivyo Simba hufanya attempts hizi kipndi ambacho hali ya msosi ni mbaya kweli kweli. Napo chance za kufanikiwa ni ndogo. Endapo sharubu atamfuma tembo mgonjwa au aliyejeruhiwa basi napo huweza kufanikiwa.
Ktk purukushani ya kumwinda tembo, Simba hukimbilia kuudaka mkonga wake, kwani simba style yake ya kuua ni kwa kumkosesha hewa adui yake - suffocation.

picha zote zimepigwa Hifadhi ya taifa ya Ruaha Nationbal park na timu ya wadau waliofanya safari yao hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment